Mapumziko ya wiki mbili kupisha mechi za kimataifa za kirafiki yamemkera kocha wa Yanga, George Lwandamina akihofia ari ya vijana wake kushuka
Lwandamina ambaye yuko nchini Zambia kuhudhuria msiba wa mpwa wake amesema kama ingekuwa amri yake ligi isingesimama kutokana na kasi waliyokuwa nayo wachezaji wake hivi sasa.
"Nivitu vya kawaida hata ulaya vinatokea, lakini kwa kipindi hiki tulichopo sikutamani mapumziko kama haya kwasababu timu tayari ilishaonyesha kuelewana na kucheza kwa kufuata maelekezo ninayowapa lakini lazima niyakubali kwakua yanatoka kwenye uongozi wa juu, " amesema Lwandamina.
Mzambia huyo amesema pamoja na hayo ataendelea na mazoezi kama kawaida na wachezaji ambao hawapo kwenye timu zao za taifa ili kuhakikisha anabakiza ile spiriti iliyokuwepo tangu katika mchezo wa mwisho waliocheza dhidi ya Singida United ambapo walitoka sare ya bila kufungana.
Kocha huyo amesema Yanga, bado inanafasi ya kufanya vizuri na kutetea ubingwa wake msimu huu hivyo bado ataendelea kuwajenga vijana wake kwa kuwapa mbinu bora ili kuhakikisha wanafanya vizuri na kutwaa taji hilo kwa mara ya nne msimu huu.

ADVERTISE HERE