Tambwe yuko tayari kucheza bure Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 May 2020
Tambwe yuko tayari kucheza bure Yanga

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Amis Tambwe, bado ana ndoto ya kurudi kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria akibainisha kuwa yuko tayari hata kucheza bure

Tambwe ambaye aliitumikia Yanga kwa misimu minne yenye mafanikio, amesema heshima aliyoitengeneza wakati akiwa na klabu hiyo, imemfanya ajihisi kuwa bado ana deni kubwa kwa Wanajangwani hao

"Yanga imenipa heshima kubwa sana na ilinifuta machozi pale nilipokuwa na maumivu, sina ambacho naweza kuwalipa zaidi ya kuwa tayari kufanya nao kazi"

"Nitafurahi nikipata nafasi nyingine ya kuitumikia Yanga kwa sababu imenipa historia kubwa na kubadili maisha yangu, natamani wanipe nafasi ya kucheza hadi nitakapostaafu mpira hata kwa kujitolea tu," Tambwe amenukuliwa na gazeti la Bingwa

Tambwe alijiunga na Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu wa 2014/15 wa Ligi Kuu Bara baada ya kutemwa na Simba dakika za mwisho

Alitoa mchango mkubwa katika misimu yote mitatu ambayo Yanga ilitwaa taji la ligi kuu mfululizo kuanzia 2014 mpaka 2017

Majeraha aliyopata mwaka 2017, yalimfanya akae nje kwa muda mrefu hali iliyopelekea kuathiri kiwango chake kwa kiasi kikubwa

Msimu wake wa mwisho alifunga mabao nane kwenye ligi. Hata hivyo aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alimnyima mkataba mpya hivyo kumfanya aondoke akiwa mchezaji huru

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’