Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amesema anatamani ligi irejee mapema ili waendelee na majukumu yao kama wachezaji kuwapa burudani mashabiki wao
Kiungo huyo mkabaji, amesema muda mrefu waliokaa nyumbani, umewafanya wakumbuke sana soka
"Ki ukweli tunaomba mungu hii corona imalizike ili tuendee na kazi yetu. Tumekaa muda mrefu, tunafanya mazoezi peke yetu tu, binafsi natamani sana kucheza mpira. Lakini tutaendelea kusubiri hadi pale watakaposema turudi tena kucheza mpira," amesema
Mcongomani huyo anaendelea na program za mazoezi zinazotolewa na kocha wake Luc Eymael ambapo yeye kama nahodha hutumiwa program zote
Amesema wachezaji wote wa Yanga wanafanya mazoezi hayo na anaamini ligi itakaporejea, benchi la ufundi halitakuwa na kazi kubwa ya kufanya