Beki wa zamani wa Yanga Hassan Kessy anayecheza klabu ya Nkana Fc ya Zambia, amesema amesikia taarifa za mabosi wake wa zamani kumuwania beki wa Kimataifa wa Kenya, Mussa Mohammed ambaye anacheza nae klabu ya Nkana
Kessy amesema kama mabingwa hao wa kihistoria wataweza kuipata saini ya Mohammed, basi watakuwa wamepata mchezaji mzuri
"Ni mmoja wa wachezaji wa kutegemewa kwenye kikosi cha Nkana, utakuwa usajili mzuri sana kwa Yanga kama watafanikiwa kumpata," amesema Kessy ambaye pia mkataba wake na Nkana unamalizika mwishoni mwa msimu
Hivi karibuni Mohammed alikiri wakala wake kufanya mazungumzo na Yanga ambayo imeonyesha nia ya kutaka kumsajili
Mchezaji huyo atakuwa huru mwishoni mwa msimu akiwa ukiongoni mwa mkataba wake
ADVERTISE HERE