Ligi ikirejea wadau kupimwa corona kila mechi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 May 2020
Ligi ikirejea wadau kupimwa corona kila mechi

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almas Kasongo amesema wamewasilisha mapendekezo yao Serikalini katika mpango wa kurejea kwa ligi kuu ya Vodacom

Kasongo amesema wamependekeza ligiΒ  irejee katika ya mwezi Juni huku wakiweka utaratibu ambao utahakikisha wahusika wote wa mechi kuanzia wachezaji, benchi la ufundi, maafisa wa mchezo na waandishi wa habari wanafanyiwa vipimo vya corona kabla ya mchezo

Kasongo amesema wanasubiri majibu ya Serikali hivyo kwa sasa ni vyema timu zikaendelea kufuata maelekezo ya Serikali kuhusiana na udhibiti wa ugonjwa wa corona

Baada ya kauli ya Rais Dk John Magufuli ambaye wiki iliyopita alidokeza kusudio lake la kuruhusu ligi hiyo kuchezwa katika mazingira salama, timu karibu zote zimeongeza mkazo kwa wachezaji wao kufanya mazoezi

"Tumependekeza utaratibu salama ambapo tutahakikisha wahusika wote wa kila mchezo wanafanyiwa vipimo vya corona. Hapa nazungumzia wachezaji, maafisa wa benchi la ufundi, maafisa wa mchezo na waandishi wa habari"

"Ni kusudio letu kuhakikisha mechi zote zinachezwa katika mazingira salama. Tunasubiri kusikia upande wa Serikali wanasemaje hivyo ni vyema timu zikaendelea kufuata maelekezo yanayotolewa, hakuna ruhusa iliyotolewa kwa timu kufanya mazoezi ya pamoja"

"Pale Serikali itakapoturuhusu, tutapanga ratiba ya muda wa mazoezi na wakati wa kuanza mechi zenyewe"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’