Tuko tayari, ligi ije tu - Niyonzima

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 May 2020
Tuko tayari, ligi ije tu - Niyonzima

Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima amesema wachezaji wote wako tayari kupambana kwenye ngwe ya lala salama ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kukata tiketi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao

Pamoja na kuwa na nafasi finyu ya kutwaa taji la Ligi Kuu, Niyonzima amesema ligi itakaporejea watapambana kuhakikisha kama wanakosa ubingwa basi wamalize nafasi ya pili

Kwa michuano ya kombe la Shirikisho la Azam, Niyonzima amesema wanahitaji kushinda taji hilo

Niyonzima ambaye siku za karibuni alijiongezea dozi ya mazoezi kwa kuweka kambi ufukweni akijifua, amesema wachezaji wote wanahimizana kufanya mazoezi wakati huu ligi imesimama ilin pale itakaporejea waweze kutimiza malengo waliyojiwekea

"Ligi itakaporejea itakuwa kama tunaanza upya msimu kwani tumekaa mda mrefu bila ya kucheza mpira. Mechi za mwanzo zitabebwa zaidi ya uwezo wa mchezaji moja mmoja sasa kwa timu ambayo wachezaji wake watakuwa wamefanya mazoezi kikamilifu, ni wazi watanufaika"

"Ndio maana sisi Yanga tuliweka mkazo mkubwa kwa kila mmoja wetu kufanya mazoezi mazuri ili tuweze kutimiza malengo tuliyojiwekea," amesema

"Pia Tunajivunia kocha wetu (Luc Eymael), amekuwa akituhimiza mara kadhaa namna ya kujiweka sawa kabla ya ligi kurejea, hivyo kila mchezaji ana hamu ya kurejea uwanjani na kusawazisha mapungufu yote yaliyojitokeza kabla ya kusimama kwa ligi, naamini tutarejea na nguvu na kuchukua Kombe la Shirikisho au kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi"

Ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao, Yanga inapaswa kushinda taji la FA kwani huenda msimu ujao Tanzania ikatoa vilabu viwili tu ikielekea kupokwa nafasi nne na Libya ambayo moja ya klabu zake ilitinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho hivyo kuizidi alama Tanzania

Lakini mambo yanaweza kuwa tofauti kama CAF wataamua kufuta matokeo ya michuano yake ya msimu baada ya mechi zote kusimamishwa kutokana na corona

CAF wamesitisha michuano ya yote ya Kimataif huku wakiwa bado hakuna taarifa rasmi waliyoitoa kuhusu mustakabali wa michuani hiyo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’