Tunawafuatilia wachezaji wote - Kandoro

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 May 2020
Tunawafuatilia wachezaji wote - Kandoro

Mkurugenzi wa Mashindano klabu ya Yanga Thabiti Kandoro amesema uongozi wa timu hiyo umeweka utaratibu wa kuwafuatilia wachezaji wake ili kuhakikisha wanatekeleza program za mazoezi waliyoachiwa na kocha Luc Eymael

Kandoro amesema wakati huu ambao ligi imesimama kutokana na ugonjwa wa corona, ni muhimu kwa wachezaji kufanya mazoezi stahiki ili kulinda viwango vyao

"Tunafuatilia mazoezi ambayo wanafanya wachezaji wetu. Meneja wa timu pamoja na Daktari wanawasiliana na wachezaji moja kwa moja. Lengo ni kuhakikisha program za Mwalimu zinatekelezwa ipasavyo"

"Tunashukuru mpaka sasa hatuna majeruhi, wachezaji wana Amani wakiendelea na progam zao vyema. Kimsingi sisi tuko tayari kwa lolote, tunachosubiri ni mwongozo wa Serikali na TFF kwani wao ndio wenye kauli ya mwisho kuhusu lini ligi itarejea," Kandoro aliiambia Yanga TV

Mapema leo, Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao alibainisha kuwa wanasubiri maelekezo ya Serikali, hivyo aliwataka wadau waendelee kuwa watulivu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’