Eymael awapotezea nyota wa Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 May 2020
Eymael awapotezea nyota wa Simba

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema malengo yao ni kuunda kikosi imara kwa kusajili wachezaji wazuri kutoka kila pembe ya Afrika

Aidha katika usajili wake, Eymael amesema hadhani kama watasajili mchezaji kutoka kwa watani zao ambao ndio wapinzani wao wakubwa, Simba

Kuna wakati Yanga ilihusishwa kuwawania nyota kadhaa wa klabu ya Simba wakianza na kiungo Clatous Chama ambaye tetesi zilianzishwa na Makamu Mwenyekiti Fredrick Mwakalebela ingawa baadae alikanusha kuwa alitania

Kauli ya Mwakalebela ilipelekea klabu ya Simba kupeleka malalamiko TFF

Eymael amesema hawatasajili mchezaji yeyote kutoka Simba kwani anafahamu hata wakimtaka mchezaji kutoka klabu hiyo, hawatakuwa tayari kuwauzia

"Simba nao wanajenga timu yao kama ilivuyo sisi, sidhani kama wanaweza kukubali kutuuzia mchezaji wao muhimu, labda mchezaji huyo awe amemaliza nao mkataba"

"Tumeingia sokoni kusaka wachezaji wa nafasi mbalimbali tulizoziona kuwa na mapungufu. Tuna uhakika tutapata wachezaji wazuri zaidi ya hao wanaotajwa kutoka Simba," amesema Eymael

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’