Winga wa AS Vita Tusila Kisinda ni mmoja wa wachezaji ambao wamekuwa wakihushwa kuwaniwa na Yanga
Inafahamika Yanga imepanga kusajili winga wa kulia ambaye atakidhi mahitaji ya kocha Luc Eymael, Kisinda akiwa pendekezo la kocha huyo Mbelgiji
Hivi karibuni nyota huyo alinukuliwa na gazeti moja maarufu nchini akikiri kufanya mazungumzo na mmoja wa mabosi wa GSM ambaye husimamia michakato ya usajili
Kisinda alibainisha kuwa walifikia mwafaka wa mazungumzo yao na kinachosubiriwa ni muda wa usajili kufika ili aweze kusaini mkataba
Katika usajili wake, huenda Yanga ikashusha nyota wawili au zaidi kutoka DR Congo kwani pia inahusihwa na washambuliaji Heritier Makambo (Horoya AC) na Mpiana Monzizi (FC Lupopo)
ADVERTISE HERE