Nyota Rayon aomba usajili Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 May 2020
Nyota Rayon aomba usajili Yanga

Wakati Yanga ikihusishwa kumuwania kiungo wa Rayon Sports, Ally Niyonzima, nyota mwingine wa timu hiyo ambaye pia hucheza nafasi ya kiungo Kakule Mughen amedai kufanya mazungumzo na Mhandisi Hersi Said, Mkurugenzi wa uwekezaji GSM ambaye husimamia michakato ya usajili ambayo iko chini ya kampuni hiyo kwa niaba ya Yanga

Kuelekea kipindi cha dirisha kubwa la usajili ambalo kama isingekuwa corona lingefunguliwa mwezi Juni, wachezaji wengi wameendelea kuhusishwa na mabingwa hao wa kihistoria ambao wametangaza kukisuka upya kikosi chao kuelekea msimu ujao

Kakule mwenye asili ya DR Congo, amefichua kuwa alimtumia mhandisi Hersi clip za video zake baada ya bosi huyo kumtaka afanye hivyo

"Mkataba wangu ya Rayon unamalizika karibuni. Nilifanya mazungumzo na mwakilishi wa GSM ambaye alinitaka nimtumie video zangu, nimemtumia. Natamani kuja kucheza mpira Tanzania, niliwahi kufanya majaribio Simba lakini mambo hayakwenda kama yalivyotarajiwa. Kwa sasa bado ni mchezaji wa Rayon lakini nasubiri majibu kutoka klabu ya Yanga", alisema Kakule

Hata hivyo nyota huyo sio miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye hesabu za kocha Luc Eymael

Rayon Sports huenda ikawapoteza wachezaji wake wengi kutokana na changamoto za kiuchumi zilizoikabili timu hiyo hata kabla ya kuibuka kwa ugonjwa wa corona

Klabu hiyo ilivunja mkataba na mshambuliaji wake tegemeo Michael Sarpong ambaye ni miongoni mwa wachezaji ambao wako kwenye rada za Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’