Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael huko aliko atakuwa anaweka mabegi yake sawa tayari kurejea nchini baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk John Magufuli kutarajiwa kufungua usafiri wa anga wiki hii
Eymael hayuko Tanzania tangu mwezi March baada ya ligi kusimama kutokana na corona akirejea kwao Ubelgiji ambako alikwenda kufunga ndoa
Mbelgiji huyo ameeleza kupokea kwa furaha tamko la Rais Magufuli akibainisha sasa anasubiri utaratibu wa kwao Ubelgiji ili aweze kurejea
Kama ilivyokuwa kwa Tanzania, nchi ya Ubelgiji nayo lifunga mipaka pamoja na kusitisha usafiri wa anga wakiiweka nchi yao kwenye lock-down kudhibiti maambukizi ya corona
Ubelgiji ilikuwa nchi ya kwanza kutangaza kumaliza msimu wao wa ligi mapema kutokana na changamoto ya corona ambao imeisimamisha dunia kwa takribani miezi miwili