Mahadhi atuma ujumbe wa kibabe Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 May 2020
Mahadhi atuma ujumbe wa kibabe Yanga

Winga wa Yanga Juma Mahadhi amesema kwa sasa amepona kabisa majeraha yake na kuwataka mashabiki wa timu hiyo wasubiri burudani kutoka kwake pale ligi itakaporejea

Mahadhi hajaonekana uwanjani kwa karibu miaka miwili akiuguza jeraha la goti alilopata August 19 2018 katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya USMA. Mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1

"Kwa sasa nipo vizuri naendelea na mazoezi binafsi. Nawaambia Mashabiki, Wanachama na wapenda soka wategemee kuniona nikirejea uwanjani ligi itakaporejea," ametamba Mahadhi

Ujio wa nyota huyo ni kama ingizo jipya kwenye kikosi cha kocha Luc Eymael, Mbelgiji huyo atamuangalia kwa jicho tofauti

Yanga imejipanga kuingia sokoni kusaka winga wa upande wa kulia, pengine itakuwa nafasi kwa Mahadhi kumuonyesha Eymael kuwa hata yeye anaimudu nafasi hiyo

Hata hivyo kwa kuwa amekaa nje kwa muda mrefu, pengine atahitaji mechi kadhaa kuweza kujiimarisha kabla ya kuonyesha makali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’