Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk John Magufuli ameruhusu michezo yote iliyokuwa imesitishwa kutokana na janga la corona ikiwemo Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Ligi daraja la Kwanza, Ligi daraja la Pili na hata michezo ya kuigiza iendelee kuanzia tarehe 01/06/2020
Aidha, Rais Magufuli ameitaka Wizara ya Afya na Wizara ya Michezo kushirikiana ili kuweka utaratibu wa tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona wakati wa mechi na michezo mingine
Sasa ni rasmi mshikemshike wa Ligi Kuu utarejea katika kipindi cha wiki mbili..
ADVERTISE HERE