Eymael ahofia atachelewa kufika Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 May 2020
Eymael ahofia atachelewa kufika Tanzania

Pamoja na uongozi wa Yanga kubainisha kuwa wameanza mchakato wa kuwarejesha makocha wao  Luc Eymael (Kocha Mkuu) na Riedoh Berdien (Kocha wa viungo), Eymael amehofia huenda atachelewa kurejea nchini kutokana na kukumbana na changamoto ya usafiri huko Ubelgiji

Mbelgiji huyo ameeleza kufurahishwa na tamko la Rais Dk John Magufuli ambaye ametangaza shughuli zote za michezo kurejea kuanzia Juni Mosi

Hata hivyo amesema nchini kwao hakuna usafiri wowote wa Ndege utakaomuwezesha kuja Tanzania kabla ya Juni Mosi, hivyo huenda atalazimika kusubiri zaidi

Ni wazi, kama TFF itatangaza kuanza kwa ligi mwanzoni mwa mwezi Juni, huenda kocha msaidizi Charles Mkwasa atakabidhiwa majukumu ya kuwaongoza mabingwa hao wa kihistoria

Yanga inakabiliwa na michezo 11 ya kumalizia msimu lakini pia wana mechi ya robo fainali michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), droo yake ikitarajiwa kupangwa wakati wowote baada ya Rais Magufuli kuruhusu michezo

Yanga imepania kushinda ubingwa wa FA ili waweze kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’