Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amesema wamekubaliana mechi zilizobaki kwa Ligi Kuu na kombe la Shirikisho (AFSC) zitapigwa jijini Dar es salaam katika viwanja vya Taifa, Uhuru na Azam Complex
Aidha kwa mechi za ligi daraja la kwanza na la pili zote zitapigwa mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba na Nyamagana
"Tumeteua vituo viwili; Mwanza, CCM Kirumba na Uwanja wa Nyamagana na Dar es salaam viwanja vya Taifa, Uhuru na Chamazi. Ligi Kuu na Azam Sport Federation Cup itabaki jijini Dar es salaam wakati ligi daraja la kwanza na la pili itafanyika jijini Mwanza," amesema Dk Mwakyembe
Hata hivyo bado TFF na Bodi ya Ligi wanasubiriwa kutoa tamko rasmi na ratiba ya mechi hizo
Β
ADVERTISE HERE