Mashabiki wasiozidi kumi kwa kila timu, wataruhusiwa kuingia uwanjani kuzishangilia timu zao wakati mikikimikiki ya ligi kuu ya Vodacom itakaporejea kuanzia Juni Mosi
Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dk Harrison Mwakyembe amesema mashabiki hao watafanyiwa vipimo vyote kuhakikisha wako salama na hata watakapoingia uwanjani, hawataruhusiwa kukaa mahali pamoja
"Kila timu itaruhusiwa kuwa na mashabiki wachache ambao hawatazidi 20 ambao watatakiwa kukaa uwanjani kwa utaratibu ambao unafuata umbali unaoelekezwa ili kuepuka maambukizi ya corona"
"Mashabiki wote watapimwa afya kabla ya kuruhusiwa kuingia uwanjani," alisema Dk Mwakyembe jana wakati akitangaza utaratibu utakaotumika wakati ligi ikirejea
Aidha pamoja na kuruhusu timu kuanza mazoezi, Waziri Mwakyembe amesema bado wanapaswa kufuata taratibu zote za kujikinda na corona ikiwa ni pamoja na kuweka umbali unaotakiwa
Pia wachezaji hawaruhusiwa kukumbatiana, kushikana mikono au kutema mate uwanjani