Ngoma matatani Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Nov 2017
Ngoma matatani Yanga
Uongozi wa Yanga umesema haukumpa ruhusa mshambuliaji wake Donald Ngoma kurejea kwao nchini Zimbabwe kujitibia kama ilivyoelezwa awali.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwassa amesisitiza kuwa Ngoma aliachwa jijini Dar es salaam na wachezaji wengine majeruhi wakati Yanga ilipokwenda kanda ya ziwa.

Mchezaji huyo bado hajarudi na tayari Mkwassa amesema atachukuliwa hatua za kinidhamu atakaporejea kwa kitendo chake cha kuondoka kambini bila ya ruhusa.

Wakati huo huo Yanga huenda ikatumia dirisha dogo la usajili kusajili washambuliaji wawili.

Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina yuko nchini Zambia alikokwenda kuhudhuria msiba wa mpwa wake, ameuagiza uongozi wa Yanga utumie dirisha dogo la usajili linalofunguliwa Jumatano ijayo kuimarisha safu ya ushambuliaji.

Yanga huenda ikasajili mshambuliaji mmoja wa Kimataifa na mmoja mzawa.

Kama hilo litafanyika, ili kuweza kupata nafasi moja ya Kimataifa, Yanga italazimika kuvunja mkataba wa mchezaji mmoja wa Kimataifa.

Tayari mlinzi wa kati raia wa DRC Fiston Kayembe amejihakikishia nafasi moja ya Kimataifa iliyokuwa imebaki kwenye kikosi cha Yanga.

Amekuwa katika kikosi hicho akifanya majaribio kwa miezi kadhaa na bila shaka atasaini mkataba wa kuitumikia Yanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’