Baada ya zoezi la vipimo vya Afya kufanyika hapo jana, kikosi cha mabingwa wa kihistoria Yanga, kinaingia kambini leo kuanza mazoezi moja kwa moja chini ya kocha msaidizi Charles Mkwasa
Awali klabu hiyo ilikuwa imepanga kuanza mazoezi Juni 01, lakini Mkwasa ameitaka timu yake ianze mazoezi leo kwa kuwa ratiba ya mechi inaweza ikawabana hasa ikitokea ligi itarejeshwa wiki ijayo
"Nimeona tuanze mazoezi mapema, tunaweza kujipanga kwa tarehe moja, halafu tukawa na ratiba ya mechi tarehe mbili, sasa tumeona vyema tukachukua tahadhari hii ya kuanza mazoezi haraka," kauli ya kocha Msaidizi wa Yanga Charles Mkwasa aliyoitoa jana
Mkwasa amesema atayatumia mazoezi ya leo kuangalia kama wachezaji walikuwa wanatekeleza program waliyopewa na kocha mkuu Luc Eymael.
"Wachezaji wote wako vizuri, tutaanza mazoezi rasmi kwa kuanza kutafuta basic endurance na ball work kidogo kwa sababu tumepata program ya kocha mkuu na tutaifanyia kazi"
"Kwenye mazoezi kuna vitu lazima tuvizingatie (fitness, technic, tactic na phycology) naamini fitness itakuwepo lakini hatuwezi kuanza mazoezi kwa speed kubwa tutaanza taratibu"
Pamoja na kupima Afya, wachezaji walikutana na uongozi kujadili mkakati wa kumaliza msimu vizuri pia kupewa taratibu za kujikinga dhidi ya Corona wakiwa mazoezini