Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa droo ya hatua ya robo fainali kombe la FA (ASFC) itafanyika kesho Ijumaa
Tukio hilo litafanyika Makao Makuu ya Azam TV, Tabata jijini Dar es salaam, saa tano asubuhi
Mechi zote zilizobaki zitapigwa jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Taifa, Uhuru na Azam Complex
Timu zilizofuzu kwa hatua hiyo ni Yanga, Simba, Azam Fc na Namungo
Nyingine ni Sahare All Stars, Kagera Sugar, Ndanda na Alliance Fc
ADVERTISE HERE