Droo ya hatua ya robo fainali michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) imefanyika leo Makao Makuu ya Azam TV, Tabata jijini Dar es salaam
Mabingwa wa kihistoria Yanga wao wamepangwa kucheza na Kagera Sugar katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Taifa
Aidha mabingwa watetezi wa michuano hiyo Azam Fc wao wamepangwa kucheza na Simba wakati Namungo Fc wao wakitarajiwa kuanzia nyumbani katika mchezo wao wa robo fainali dhidi ya Alliance Fc
Sahare All Stars timu pekee ya daraja la kwanza iliyopenya hatua ya robo fainali, itachuana na Ndanda katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Mkwakwani
Mechi za robo fainali zitapigwa tarehe 27/28 Juni na hatua ya nusu fainali ikitarajiwa kupigwa mwezi wa saba
ADVERTISE HERE