Huenda mashabiki wataruhusiwa kushuhudia mechi za ligi kuu viwanja baada ya Serikali kutoa muongoza unaoelekeza utaratibu wa kufuatwa katika kuendesha michezo iliyoruhusiwa
Kulingana na mwongozo uliotolewa na Serikali, umevitaka vyama vinavyosimamia mchezo kuhakikisha vinazingatia tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa wa corona
Aidha yapo maelekezo ambayo TFF inatakiwa kuhakikisha mashabiki watakaoruhusiwa kuingia viwanjani wanakaa umbali wa mita moja
Hii ni habari njema kwa mashabiki wa soka nchini kwani tamko la awali lilikuwa limetoa maelekezo ya mashabiki 20 (10 kwa kila timu) ambao wangeruhusiwa kuingia uwanjani
ADVERTISE HERE