Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema kikosi chao kimepokea kwa furaha droo ya hatua ya robo fainali kombe la FA, ambapo wamepangwa na Kagera Sugar katika mchezo ambao utapigwa Juni 27/28 uwanja wa Taifa
Bumbuli amesema wamefurahi kukutana tena na Kagera Sugar kwani hii itakuwa nafasi yao kulipa kisasi
Yanga ilicheza na Kagera Sugar katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu na kukubali kipigo cha mabao 3-0
Nugaz aliwataka Simba
Nae Afisa Mhamasishaji wa klabu hiyo Antonio Nugaz amesema yeye alitamani wangeanza na Simba katika hatua hii ya robo fainali
Hata hivyo amesema watahakikisha wanapata ushindi dhidi ya Kagera Sugar ili watinge nusu fainali hatua ambayo wanaweza kukutana na Simba kama nayo itafanikiwa kuifunga Azam Fc
Mechi nyingine za robo fainali ni kati ya Namungo Fc dhidi ya Alliance na Sahare All Stars dhidi ya Ndanda