Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde ni miongoni mwa wageni walioalikwa kushuhudia tukio la kusainiwa mkataba wa ushirikiano kati ya Yanga na La Liga kuelekea mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Yanga
Uongozi wa Yanga umeeleza kutambua mchango mkubwa wa Mavunde ambaye Kamati yake ya Hamasa ilikuwa mwanzo wa safari ya mabadiliko inayokwenda kutambulishwa rasmi leo

"Mheshimiwa Anthony Mavunde ni mmoja wa kiongozi ambaye ameshiriki kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha heshima ya Klabu hii inatunzwa"
"Aliongoza kamati ya HAMASA akiwa na wajumbe wake kwa MAFANIKIO makubwa sana. Leo tunashuhudia safari ya mabadiliko makubwa sana ya Yanga ambayo yana mkono wenu wewe na wajumbe wa kamati yako"
"Ni furaha kwetu leo kujumuika na wewe kwenye hafla ya Utiaji saini wa Mchakato wa mabadiliko ya kiundeshaji wa Klabu ya Yanga," imesema taarifa ya Yanga