Bado wapo watu wachache 'wenye roho ngumu' kuwa hawaamini kama Yanga imeingia makubaliano na La Liga ambayo yanakwenda kuifanya taasisi hiyo kujiendesha kisasa na kuongeza thamani yake
Baadhi walifikia kuhoji mbona La Liga hawajaposti jambo lolote kuhusu mkataba huo kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii
Sasa kupitia ukurasa wao wa Facebook, La Liga wametoa taarifa rasmi kuhusu mkataba waliosaini na klabu ya Yanga pamoja na Sevilla

Ukurasa wa La Liga mtandao wa Facebook una wafuasi zaidi ya Milioni 63, ndio ukurasa wenye wafuasi wengi zaidi kuliko kurasa zao nyingine
Idadi hiyo ni kubwa kuliko wananchi wote wa Tanzania! Ni hatua mojawapo katika kuitangaza Yanga huko duniani
ADVERTISE HERE