Wadhamini wa Ligi Kuu, kampuni ya Vodacom na Azam Tv wanatarajiwa kutoa kitita cha fedha kwa vilabu vinayoshiriki ligi hiyo kuelekea ngwe ya mwisho ya kumaliza msimu
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Steven Mguto amesema Vodacom wanatarajiwa kutoa mgawo wa Tsh Milioni 23 wakati Azam Tv wao watatoa mgawo wa Tsh Milioni 44
Fedha hizo ni sehemu ya fedha za udhamini ambazo zimekuwa zikitolewa kwa awamu
Mguto amesema fedha hizo zitavisaidia vilabu kufanya maandalizi na kumaliza msimu vyema
Wakati wa mapumziko ya corona, Vodacom ilitoa tsh Milioni 23 pia
ADVERTISE HERE