Kesho Jumapili, kikosi cha Yanga kitashuka kwenye uwanja wa Uhuru kumenyana na KMC ukiwa ni mchezo wa kirafiki kujiandaa na kurejea kwa mikiki mikiki ya ligi kuu wiki ijayo
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli ametaja viingilio vya mchezo huo kuwa ni Tsh 5,000/- VIP na Mzunguuko ni Tsh 3,000/-
Bumbuli amesema wameweka viingilio rafiki ili kuwapa nafasi mashabiki wengi kuishuhudia timu yao kwa mara ya kwanza baada ya kukosa burudani kwa miezi miwili kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona
Aidha Bumbuli amesema Yanga imechukua tahadhari zote na kuhakikisha wanazingatia maelekezo yaliyotolewa na Serikali kujilinda na maambukizi ya corona
"Mashabiki wanaokuja uwanjani ni lazima wavae barakoa, watapita kwenye mageti maalum ambayo yatakuwa na vitakasa mikono," alisema