Kiungo mkabaji wa Yanga Abdulaziz Makame jana alipata majerahai kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC ambao ulimalizika kwa Yanga kufungwa mabao 3-0
Tangu kuanza kwa mwaka 2020, Makame amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kutokana na majeraha yanayomsumbua mara kwa mara
Ni kama jana alitonesha jeraha la goti ambalo limekuwa likimkosesha fursa ya kudhihirisha ubora wake
Kuingia kwake katika mchezo huo, kuliimarisha safu ya kiungo cha chini ambayo awali alikuwa akicheza Said Juma Makapu ambaye alirudishwa nafasi ya ulinzi
Alionyesha kiwango kizuri katika dakika chache alizocheza kabla ya kutolewa baada ya kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo
Yeye pamoja na mkongwe Mrisho Ngasa, walipoingia waliichangamsha Yanga ambayo ilicheza chini ya kiwango katika mchezo huo