Kiungo wa Yanga Feisal Salim 'Fei Toto' amewatuliza mashabiki wa timu hiyo kufuatia kipigo cha mabao 3-0 hapo jana kutoka kwa KMC katika mchezo wa kirafiki
Fei Toto amesema hata wao wameumia kupoteza mchezo huo lakini ndio matokeo ya mpira
Aidha kiungo huyo kutoka visiwani Zanzibar amesema watasahihisha makosa yaliyojitokeza kuelekea mchezo dhidi ya Mwadui Fc
"Ni matokeo ambayo hakuna aliyetarajia, hata sisi wachezaji tumeumia lakini ndio mpira wa miguu ulivyo, matokeo huwa ni matatu, kufungwa, kushinda au kutoka sare. Sie kufungwa haimaanishi kuwa timu yetu ni mbovu, ni mchezo tu," alisema
"Muhimu tuendelee kumuomba Mungu kwani kila kitu kitakuwa sawa"
Jumamosi ya wiki hii Yanga itaelekea mkoani Shinyanga kuikabili Mwadui Fc katika mchezo wa ufunguzi baada ya ligi kurejea