Stars yaibana mbavu Benin

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Nov 2017
Stars yaibana mbavu Benin
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeibana Benin kwenye dimba lake la nyumbani kwa kuilazimisha sare ya bao 1-1.

Benin ilianza kupata bao la kuongoza kwenye kipindi cha kwanza mfungaji akiwa winga wa zamani wa Sunderland Stephan Sessegnon kupitia mkwaju wa penati.

Hata hivyo, ilikuwa ni penalti ya mashaka, kwani mchezaji aliyeugusa mpira huo kwa mkono alikuwa ni wa Benin, Khaled Adenon lakini refa akadhani ni mchezaji wa Tanzania.

Benin ilitawala mchezo huo katika kipindi cha kwanza hata hivyo Stars ilibadilika kwenye kipindi cha pili ambapo ilifanikiwa kusawazisha bao kwenye dakika ya 55 mfungaji akiwa Elias Maguri.

Maguri aliupachika mpira kimiani akiunganisha vyema krosi ya Shiza Kichuya aliyewatoka walinzi na kumimina majaro kutoka upande wa kushoto.

Matokeo haya yanaweza kuisaidia Starskupanda ja[po kidogo kwenye viwango vya FIFA kwani Benin iko nafasi ya 78.

Kikosi cha Benin kilikuwa; Fabien Farnole, Rodrigue Fassinou, Khaled Adenon, Cedric Hountonji, David Kiki, Djiman Koukou, Olivier Verdon, Jodel Dossou, Stephane Sessegnon, David Djigla Dossou na Steve Mounie.

Tanzania; Aishi Manula, Himid Mao, Gardiel Michael, Abdi Banda, Kelvin Yondan, Hamisi Abdallah/Jonas Mkude dk75, Simon Msuva/Boniphace Maganga dk85, Mudathir Yahya/Nurdin Chona dk92, Elias Maguli, Raphael Daudi/Mbaraka Yusuph dk54 na Shizza Kichuya/Ibrahim Ajib dk65.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’