Licha ya kuanza mazoezi jana, nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi hatajumuishwa kwenye safari ya mkoani Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa Jumamosi, Juni 13 kwenye uwanja wa CCM Kambarage
Kocha msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema Tshishimbi atabaki Dar ili aendelee kuimarika tayari kwa michezo ijayo.
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kupaa kwa Ndege mpaka jijini Mwanza kisha kuchukua usafiri wa basi kuelekea mkoani Shinyanga kwa ajili mchezo huo wa ufunguzi baada ya ligi kurejea
ADVERTISE HERE