Majeraha yanavyomtesa Tambwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Nov 2017
Majeraha yanavyomtesa Tambwe
Mchana nyavu mahiri wa Yanga Mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe, amesema kuwa kukaa nje muda mrefu Kunamfanya awe na hamu ya kurudi uwanjani kwa kasi.

Tambwe aliyetokea klabu ya Vitalo ya Burundi kabla ya kujiunga na Simba, ameshawahi kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara akiwa na timu mbili tofauti.

Kwenye mahojiano na mtandao wa GOAL, Tambwe amesema amekuwa akiifuatilia kwa karibu timu yake na kupatwa na midadi Jambo ambalo linalomfanya awazie kurudi dimbani ili kusaidiana na wachezaji wenzake katika kuipigania mafanikio ya mabingwa hao.

"Naumia sana kuona nipo nje na wenzangu wanaendelea kupigika, ninachokwambia kwasasa ni kurudi kazini mapema iwezekanavyo ili kuungana na wenzangu tuweze kuipigania timu yetu kwa Mara ya nne mfululizo."

Mshambuliaji huyo raia wa Burundi amesema kazi kubwa tayari ameanza mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiandaa na mechi zinazofuata lakini kitu cha msingi ambacho kipo mbele yake ni kuangazia namna ya kuongeza nguvu wakati huu ambapo Ligi imekuwa na ushindani mkubwa.

Amesema kwa Mtazamo wake Yanga bado ni timu imara nchini na inauwezo wa kufanya vizuri hata kwenye michuano ya kimataifa hivyo kitu cha msingi ni maandalizi mazuri ili waweze kutimiza malengo ya timu.

Tambwe hajaichezea Yanga tangu kuanza kwa msimu huu na tatizo kubwa linalomkabili ni maumivu ya got aliyapata kisiwani Pemba wakati wakijiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’