Mashabiki wa klabu ya Yanga wameutaka uongozi wa timu hiyo kuangalia namna wanaweza kuichukulia hatua klabu ya Simba kwa kujaribu kumsajili kiungo mshambuliaji Bernard Morrison ambaye mwezi uliopita aliongeza mkataba wa miaka miwili
Morrison amethibitisha Simba wanamfuatilia kupitia Wakala waliompa jukumu hilo wakitaka asaini katika klabu yao ambapo amefichua kupewa dola elfu tano kama 'kishika uchumba'
"Kama Simba walimchukulia hatua Makamu Mwenyekiti wetu (Mwakalebela) kwa kauli tu tena isiyokuwa na ushahidi, sisi tunayo kila sababu ya kwenda kuwashitaki FIFA kwani ushahidi tunao"
"Tukio la Morrison sio la kufumbiwa macho kwani wao walianza kwa Chama, sisi tumalize kabisa," alisema Rashid mdau wa Mwanajangwani
Inaelezwa tukio hilo limewakera GSM ambao ndio waliomleta Morrison nchini pamoja na kusimamia mchakato wa kumuongeza mkataba
Hivi karibuni Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said alisisitiza kuwa hakuna mchezaji ambaye anahitajika Yanga ataondoka, lakini pia watasajili mchezaji yeyote kutoka ndani ya ardhi ya Tanzania ambaye kocha Luc Eymae atamuhitaji