Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema waamuzi wameendelea kutoitendea haki timu yake katika mechi za ligi kuu ya Vodacom
Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa uwanja wa Jamhuri jana na kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1, Eymael alisema wachezaji wake walifanyiwa matukio mengi yasiyo ya kiungwana na wapinzani wao lakini waamuzi hawakuchukua hatua yoyote
"Bado siridhishwi na waamuzi, wanafanya makosa mengi katika michezo yetu. Sina tatizo na kadi nyekundu aliyopewa Lamine lakini katika vurugu zilizotokea kuna wachezaji wetu walipigwa na wachezaji wa JKT Tanzania lakini waamuzi hawakuchukua hatua"
"Wiki iliyopita Azam Tv walichambua vizuri bao halali tulilonyimwa na waamuzi kwenye mchezo dhidi ya Mwadui Fc. Haya matukio yamekuwa yakijitokeza karibu kila mchezo wetu"
"Leo mmeshuhudia rafu na matukio mengi ya kibabe dhidi ya wachezaji wetu lakini hakuna hatua zilizochukuliwa badala yake tunaadhibiwa sisi kwa sababu tu mchezo unaofuata tunacheza na Azam FC," alisema
Kadi nyekundu aliyopata Lamine itamfanya akose michezo mitatu akianza na mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Jumapili Juni 21 2020