Katika kipindi cha miaka ya karibuni haikumbukwi kama Yanga imewahi kusuasua katika ligi kama ilivyotokea msimu huu
Msimu uliopita Yanga ilikuwa na hali mbaya sana ya kiuchumi lakini cha kushangazwa ilifanya vizuri kuliko wakati huu mambo yakianza kuwa sawa
Msimu huu ndio msimu ambao Yanga imefunga mabao machache sana lakini pia ikiruhusu mabao mengi
Mabao 33 yamewekwa kambani huku mabingwa hao wa kihistoria wakiruhusu mabao 21 katika nyavu zao, tofauti ya mabao 12!
Lakini pia kinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga David Molinga amefunga mabao nane tu huku akifuatiwa na Patrick Sibomana aliyefunga mabao sita
Huu ndio msimu ambao Yanga imepata matokeo mengi ya sare (sare 11), wakishinda mechi 15 na kupoteza michezo minne
Ni katika msimu huu Yanga haijafanikiwa kushika nafasi ya kwanza hata kwa dakika moja. Mashabiki walianza kuonja machungu tangu mchezo wa kwanza kabisa, wakipoteza dhidi ya Ruvu Shooting kwa kufungwa bao 1-0
Ni takwimu zisizopendeza ukilinganisha na ukubwa wa Yanga lakini ni takwimu ambazo zinapaswa kuwaamsha viongozi wa Yanga kuelekea msimu ujao
Mabadiliko ya bendhi la ufundi katikati ya msimu pamoja na mabadiliko ya wachezaji, kwa kiasi kikubwa yamechangia timu kukosa muunganiko
Baadhi ya nyota waliosajiliwa wameshindwa kuipa mafanikio timu hiyo yenye historia ya kipekee katika soka la Tanzania