Baada ya kulazimishwa matokeo ya suluhu ya bila ya kufungana juzi, kesho Jumatano Yanga itarejea uwanja wa Taifa kuumana na Namungo Fc katika mchezo ambao matokeo tofauti na ushindi yanaweza kuwaweka mabingwa hao wa kihistoria katika nafasi ngumu katika vita ya kuwania nafasi ya pili
Yanga iko nyuma ya Azam Fc kwa alama mbili, huku ikiwa mbele ya Namungo Fc kwa alama mbili pia
Hivyo ni mchezo ambao utakuwa na upinzani mkali
Timu hizo zilipokutana Ruangwa katika mchezo wa duru la kwanza, zilitoka sare ya bao 1-1
Yanga imeshindwa kupata ushindi katika michezo miwili iliyopita, ikiwa tayari imetoka sare 11 msimu huu
Wakati Yanga ikibaki jijini Dar es salaam, Azam Fc imesafiri mkoani Kagera kuivaa Kagera Sugar
ADVERTISE HERE