Niyonzima, mchezaji wa mfano Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jun 2020
Niyonzima, mchezaji wa mfano Yanga

Tangu arejee kwenye kikosi cha Yanga mwezi Januari, kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima, ameiongoza Yanga kwa vitendo

Niyonzima amedhihirisha kuwa kwa hakika ilikuwa bahati mbaya kwake kwenda kucheza kule upande wa pili

Ni mchezaji anayeonyesha mapenzi dhahiri kwa Yanga, anajituma na kutaka kuona Yanga inafanya vizuri

Amekuwa kiongozi ndani na nje ya uwanja. Ni mhamasishaji wa wenzake na huonekana kuumia pale mambo yanapokuwa hayaendi sawa uwanjani

Juhudi zake zilionekana jana kwenye mchezo dhidi ya Namungo Fc. Wakati mwingine alionekana kuwa mkali kwa wenzake lakini kwa hakika ni kutokana na kuumizwa na kile kilichokuwa kikiendelea uwanjani

Katika moja ya mahojiano yake, Niyonzima alinukuliwa akisema,  asingekuwa na furaha maishani mwake kama asingerudi kuitumikia Yanga

"Wakati nakubali kurudi Yanga nilifahamu kabisa changamoto zilizoko, lakini nafsi yangu ilikuwa ikiniambia kama sitarudi kucheza Yanga sitakuwa na furaha. Lengo langu ni kutaka kuona mchango wangu unaisaidia Yanga kupiga hatua kutoka hapa ilipo," alisema

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
48m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’