Kikosi cha Yanga kesho Jumamosi, kitashuka kwenye uwanja wa Taifa kumenyana na Ndanda Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Ni mchezo ambao mabingwa hao wa kihistoria wanahitaji matokeo ya ushindi hasa baada ya kulazimishwa sare katika michezo mitatu iliyopita
Wachezaji wa Yanga jana walifanya kikao na kuweka mkakati wa kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo huo na mingine yote iliyobaki
Baada ya Simba kujihakikishia ubingwa, Yanga inahitaji kumaliza msimu kwa heshima, angalau kumaliza katika nafasi ya pili
Hesabu kali wamezihamishia kwenye michuano ya kombe la FA ambayo wanahitaji kushinda ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao
Jumanne Juni 30, Yanga itachuana na Kagera Sugar katika mchezo wa robo fainali ambao utapigwa uwanja wa Taifa