Beki kisiki mkongwe Kelvin Yondani amesema wanauchukulia kwa umuhimu mkubwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ndanda Fc ambao utapigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa
Yondani amesema, baada ya kupoteza nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu, wanahitaji kupambana ili kumaliza katika nafasi ya pili
"Ni muhimu sana kwetu kushinda Mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda Fc ili tusogee mbele na tuwe kwenye mbio za kushika nafasi ya pili," amesema
Nae nahodha Msaidizi Juma Abdul amesema wachezaji wote watapambana kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu kesho
"Kila mmoja wetu atapambana kwa Kadra ya Uwezo wake Ili tuhakikishe tunapata ushindi kwenye Mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda Fc"
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi jioni ambapo viingilio VIP A ni Tsh 15,000/- , B&C Tsh 10,000/- na mzunguko ni Tsh 5,000/-