Mshambuliaji wa Yanga David Molinga, atajiunga na RS Berkane ya Morocco baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika mwezi August
Mazungumzo ya nyota huyo kutimkia Morocco yamekamilika na kinachosubiriwa ni mkataba wake kuhitimishwa kunako klabu ya Yanga
RS Bekane ni moja ya vilabu tishio kule Morocco msimu uliopita wakitinga fainali ya michuano ya kombe la Shirikishisho barani Afrika ambapo walifungwa na Zamalek kwa mikwaju ya penati
Molinga ameitumikia Yanga kwa msimu mmoja tu, ameshindwa kuwa na ushawishi kwa mashabiki wa mabingwa hao wa kihistoria
Mpaka sasa ameifungia Yanga mabao 11, mabao 10 kwenye ligi na bao moja kwenye michuano ya kombe la Shirikisho la Azam Fc
Ni juzi tu aliiongoza Yanga kupindua matokeo dhidi ya Namungo Fc baada ya kutokea nyuma na kupata sare ya mabao 2-2 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa
Ni Molinga aliyepachika mabao yote ya Yanga
Kila la kheri mwamba...!