Mabingwa wa kihistoria Yanga leo wamelazimika kutokea nyuma na kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ndanda Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa
Deus Kaseke aliyekuwa na siku nzuri leo, alitangulia kuifungia Yanga mapema tu kwenye dakika ya sita akiunganisha kwa kichwa krosi ya Ditram Nchimbi
Hata hivyo Ndanda walipata mabao mawili ya haraka haraka kupitia kwa Abdul Khamis na Omari Mponda
Lakini Kaseke akairudisha mchezoni Yanga kwenye dakika za lala salama kipindi cha kwanza kabla ya pacha wake, Mrisho Ngasa hajafunga bao la ushindi kwenye dakika ya 74
Ushindi huo umeipandisha Yanga mpaka nafasi ya pili baada ya Azam Fc kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Biashara United
Yanga imefikisha alama 60 wakati Azam imebakia na alama 59
ADVERTISE HERE