Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael ameipongeza klabu ya Simba kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu
Mbelgiji huyo amekiri kuwa isingekuwa rahisi kwa kikosi chake ambacho kinashika nafasi ya pili kuibuka na taji hilo

Simba ni kama imejibu mapigo ya Yanga ambayo ilitwaa taji hili kwa misimu mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka 2017
Hata hivyo Yanga inaendelea kuwa mabingwa wa kihistoria kwani wametwaa taji hilo mara 27 huku Simba ikifikisha taji la 21
Yanga imepania kurejea kivingine msimu ujao. Jambo muhimu kwa kocha Luc Eymael ni kuhakikisha anatengeneza kikosi cha ushindani
GSM wameweka kitita cha kutosha mezani kwa ajili ya kukiboresha kikosi cha Yanga kuelekea msimu ujao
ADVERTISE HERE