Baada ya ushindi dhidi ya Ndanda Fc, kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa robo fainali kombe la FA (ASFC) dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa kesho Jumanne kwenye uwanja wa Taifa
Yanga imeweka nguvu zake zote kwenye michuano hiyo kuhakikisha wanatinga nusu fainali ambako wanaweza kukutana tena na watani zao Simba kama nao watashinda mchezo wao dhidi ya Azam Fc

Yanga inapaswa kutwaa taji hilo ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao
Β
ADVERTISE HERE