Yanga vs Kagera Sugar, mechi ya kisasi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Jun 2020
Yanga vs Kagera Sugar, mechi ya kisasi

Mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga leo watashuka katika uwanja wa Taifa kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa robo fainali michuano ya kombe la Shirikisho (ASFC) ambao utapigwa kuanzia saa moja usiku

Huu ni mchezo muhimu sana kwa Yanga ambayo inasaka nafasi ya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo ikijiwekea mpango wa kucheza fainali na hatimaye kutwaa ubingwa ili kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Shirikisho CAF msimu ujao

Yanga ilijichimbia kambini baada ya mchezo dhidi ya Ndanda Mbelgiji Luc Eymael akiahidi soka la ushindani dhidi ya wapinzani wake

Ni mchezo wa kisasi kwa Yanga kwani mara ya mwisho timu hizi zilipokutana kwenye ligi, Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0

Viingilio vya mchezo huo VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kuipa nguvu timu yao katika mchezo huo ambao wamepania kushinda

Wapinzani wao Kagera Sugar walitua jijini Dar es salaam juzi usiku

Mkufunzi wa timu hiyo Meckie Mexime, alisema pamoja na kuwa wamebanwa na ratiba, wamejipanga kufanya vizuri kwenye mchezo huo

"Tulifika Dar jana (juzi) saa tatu usiku, tumekuwa tukicheza mechi kila baada ya siku mbili hivyo hilo halitusumbui. Tumepata nafasi ya kufanya mazoezi mepesi, tuko tayari kwa mchezo huo ambao tunafahamu hautakuwa mwepesi"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’