Nyota Yanga waipania Kagera Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Jun 2020
Nyota Yanga waipania Kagera Sugar

Mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho Azam (ASFC) kati ya Yanga dhidi ya Kagera Sugar unatarajiwa kuwa na ushindani mkali hasa kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo kwenye ligi

Yanga itakuwa na kila sababu ya kusaka ushindi kwenye mchezo huo ili kujihakikishia nafasi ya kutinga nusu fainali

Ni juzi tu Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi hivyo Yanga wanafahamu ni ubingwa wa FA pekee ambao utawapa nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao

Wachezaji wa Yanga wametamba kuwa leo watakata tiketi ya kutinga nusu fainali kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Kagera Sugar

Winga Deus Kaseke ambaye kwa sisi yuko katika kiwango bora, amesema wamefanya maandalizi ya kutosha ambayo yanawapa matumaini ya kufanya vizuri leo

Amesema hadhani kama Kagera Sugar watawasumbua kama walivyofanya katika mchezo wa ligi kwani kwa sasa wako vizuri kulinganisha na walivyokutana nao mwezi Januari

Naye beki Said Juma Makapu amesema mchezo wa leo hautakuwa mwepesi na ni lazima utoe mshindi. Anaamini wataweza kuwapa furaha mashabiki wao kwa kutinga nusu fainali

Aidha, Mkufunzi wa Yanga Luc Eymael amesema kikosi chake kimejipanga na kuwahakikishia wapinzani wao kuwa zama za kuendelea kuwa mteja wa Kagera Sugar zimepita na sasa wanataka kuandika historia mpya.

"Tunaingia kwenye mchezo muhimu ambao unahisia nyingi kutoka kwa mashabiki, hasa wakiwa na kumbukumbu ya kutoka kutufunga mabao 3-0 tulipokutana kwenye mchezo wa ligi, lakini niwaambie tu mashabiki watulie, kwani zama za kuendeleza uteja zimeisha tutaingia kwa lengo la kutafuta ushindi tu"

"Tumefanya maandalizi ya kutosha, ikiwemo kufanyia kazi sehemu ya ushambuliaji na ushindi tulioupata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Ndanda umetuongezea ari ya ushindi katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar," amesema

Yanga leo itakuwa na huduma ya beki wake kisiki Lamine Moro ambaye alikosa michezo mitatu kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania

Lakini pia Eymael anaweza kumtumia winga Bernard Morrison ambaye amemaliza adhabu ya kufungiwa mechi mbili

Pamoja na kuibuka mvutano baina yake na uongozi wa Yanga hivi karibuni kuhusu suala la mkataba, Morrison anaweza kujumuishwa katika kikosi cha leo kama itampendeza Eymael

hata hivyo Yanga huenda ikaendelea kukosa huduma ya nahodha wake Papy Tshishimbi ambaye aliongezewa muda wa mapumziko ili aweze kupona majeraha yanayomsumbua

Mkongwe Kelvin Yondani ambaye alifanya vizuri katika mechi za ligi alizotumika kama kiungo mkabaji, anaweza kurejeshwa katika eneo hilo akimpisha Moro katika nafasi ya ulinzi

Bila shaka, Haruna Niyonzima na Feisal Salum wataendelea kuongoza dimba la kati wakati Deus Kaseke ambaye kwa sasa anauwasha moto kwelikweli, huenda akaendelea kuimiliki nafasi ya winga wa kulia

Molinga na Nchimbi wamekuwa wakipokezana nafasi ya ushambuliaji, Nchimbi alitumika kama winga wa kushoto kwenye mchezo dhidi ya Ndanda Fc

Kazi inabaki kwa Eymael kuamua nani aanze nae kwenye mchezo huo muhimu kwa kikosi chake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’