Yusufu Mhilu, huyu ni wa kuchungwa sana leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Jun 2020
Yusufu Mhilu, huyu ni wa kuchungwa sana leo

Yanga leo inaingia uwanja wa Taifa kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa robo fainali kombe la FA ambao utapigwa saa moja jioni

Wakati hesabu za mabingwa hao wa kihistoria zikiwa katika ushindi ili kusonga mbele hatua ya nusu fainali, safu ya ulinzi inapaswa kuwa makini kuwachunga washambuliaji wa Kagera Sugar ambayo wanaongozwa na Yusufu Mhilu nyota wa zamani wa Yanga

Mhilu ndiye 'injini' ya mabao ya Kagera Sugar akiwa amefunga jumla ya mabao 16 katika michuano yote pamoja na kutoa pasi nne za mabao

Huyu ndiye mchezaji hatari zaidi kwenye kikosi cha Kagera Sugar. Katika mchezo wa ligi ambao Kagera Sugar ilishinda mabao 3-0, Mhilu alifunga moja ya mabao hayo

Aidha kuwepo kwa tetesi kuwa Yanga imeanza jitihada za kumrejesha jangwani, ni dhahiri atapania kung'ara katika mchezo huu ili kuwahakikishia mabosi wa Yanga kuwa hawatafanya makosa kumrejesha 'nyumbani'

Lakini pia Kagera Sugar wamekuwa na ubora katika safu yao ya kiungo kama ilivyo Yanga

Hivyo hili ni eneo jingine ambalo litakuwa na ushindani mkali

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’