Ngoma haijui Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Nov 2017
Ngoma haijui Yanga
Mshambuliaji raia wa Zimbabwe Donald Ngoma ameingia katika mgogoro na uongozi wa Yanga baada ya kuondoka nchini bila ruhusa.

Ngoma aliyetarajiwa kurejea jana, anadai aliruhusiwa na kocha George Lwandamina arudi kwao Zimbabwe kushughulikia matatizo ya kifamilia na kujitibu majeraha ya nyama za paja.

Uongozi wa Yanga tayari umeweka wazi kuwa mchezaji huyo atalazimika kujieleza kwa nini asichukuliwa hatua za kinidhamu kwa kitendo chake cha kuondoka kambini bila kupata ruhusa rasmi.

Huyu Donald Ngoma haifahamu vizuri klabu ya Yanga.

Kwa miaka mingi Yanga imekuwa na msimamo thabiti dhidi ya wachezaji ambao wanafanya utovu wa nidhamu wa mara kwa mara.

Kwenye miaka ya 90 Yanga ilishawahi kutimua wachezaji karibu wote wa kikosi cha kwanza baada ya kubaini walikuwa hawajitumi kwa ajili ya klabu.

Ni kipindi hicho waliibuliwa wachezaji kama Nonda Shabani, Constantine Kimanda, Maalim Salehe 'Romario' na akina Said Swedi 'scurd' baada ya kufanyika usajili mpya uliohusisha wachezaji wengi wa Yanga B.

Ni mwaka juzi tu 2015, kiungo Haruna Niyonzima alitimuliwa na Yanga kutokana na matatizo ya utovu wa nidhamu.

Niyonzima alituhumiwa kuondoka kimyakimya kujiunga na timu ya Taifa ya Rwanda na kisha kubakia huko bila kutoa taarifa yoyote licha mashindano kumalizika.

Niyonzima alilazimika kuwaomba msamaha mashabiki na wanachama wa Yanga kupitia vyombo vya habari kabla uongozi hujaamua kumsamehe.

Yanga ni klabu kubwa, na imekuwa na historia ya kipekee. Haijawahi kutokea mchezaji akajiona yeye ni zaidi ya klabu na anaweza kujiamulia mambo vyovyote atakavyo.

Ngoma ni miongoni mwa wachezaji ambao 'walipata bahati ya mtende' kusainishwa mkataba mpya mwanzoni mwa msimu.

Viongozi waliweka imani kutokana na uwezo wake, anastahili kupewa nafasi nyingine lakini inaonekana yeye hathamini imani hiyo ya viongozi kwake.

Haruna Niyonzima na Vicent Bossou wangeweza kupewa mikataba mipya na Yanga kwa kuwa walikuwa wachezaji muhimu lakini uongozi uliamua kuachana nao baada ya kuleta 'maringo'.

Huyu Donald Ngoma anaramba asali kwa ncha ya kisu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’