Faini nyingine yatua Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jul 2020
Faini nyingine yatua Yanga

Kamati ya Saa 72 Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeipiga Yanga faini ya Tsh 500,000/- kufuatia mashabiki wake kuwarushia chupa za maji wachezaji wa Namungo Fc kwenye mchezo wa ligi kuu uliopigwa wiki iliyopita.

Kamati hiyo imetoa adhabu mbalimbali kulingana na makosa yaliyofanyika kwenye mechi za Ligi Kuu zilizochezwa karibuni

Mechi namba 303: Young Africans SC 2 v Namungo FC 2

Timu ya Young Africans SC imepigwa faini ya shilingi laki tano (500,000) kwa kosa la Washabiki wake kuwarushia chupa za maji wachezaji wa Namungo walipokuwa wanashangilia baada ya kufunga goli la pili.

Tukio hilo lilitokea baada ya wachezaji wa Namungo FC kushangilia na kupita karibu na walipokaa washabiki wa Young Africans katika mechi iliyochezwa Juni 23, 2020 kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam

Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 43(1) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa Klabu

Mechi namba 300: Young Africans SC 0 v Azam FC 0

Waamuzi Elly Sasii, Sudi Lila na Mbaraka Haule wanafungiwa miezi mitatu kwa kosa la kutokuumudu mchezo uliochezwa Juni 21, 2020 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam

Adhabu hii imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 39(1) kuhusu udhibiti wa waamuzi

Mechi namba 315: Biashara United FC 1 v Azam FC 1

Timu ya Azam FC imepigwa faini ya shilingi laki tano (500,000) kwa kosa la wachezaji na maofisa wa timu hiyo kuingia uwanjani kwa kupitia lango tofauti na lililoandaliwa kwa kisingizio kwamba walizuiwa kuingia kupitia mlango elekezwa katika mechi iliyochezwa Juni 23, 2020 kwenye uwanja wa Karume Mkoani Mara.

Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 14(49) kuhusu taratibu za mchezo

Mechi namba 320: Kagera FC 1 v KMC FC 1

Timu ya KMC FC imepigwa faini ya shilingi laki tano (500,000) kwa kosa la wachezaji wake watano kuonyeshwa kadi za njano sita na nyekundu moja katika mchezo uliochezwa Juni 28,2020 kwenye uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.

Adhabu hii imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 43(10) kuhusu udhibiti wa klabu.

Mechi namba 317: Tanzania Prisons FC 0 v Simba SC 0

Kamati imetoa Onyo kali kwa Uwanja wa Sokoine, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya na klabu zote zinazotumia uwanja wa Sokoine kama uwanja wa nyumbani kwa kosa la washabiki kuingia uwanjani baada ya mchezo kumalizika.

Kamati inawataka Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya, wamiliki wa uwanja wa Sokoine na klabu zote zinazotumia uwanja wa Sokoine kuhakikisha zinazingatia kanuni ya 14(10), 14(11),14(42) na 14(43) inayohusu taratibu za mchezo inayosema:-

"Ni marufuku kwa viongozi kuingia uwanjani(pitch) bila sababu za msingi kinyume na taratibu za mchezo kabla, wakati au baada ya mchezo"

"Ni marufuku kwa mashabiki kuingia uwanjani kabla,wakati au baada ya mchezo"

"Katika mchezo wowote wa ligi kuu wakati mchezo ukiwa unachezwa hairuhusiwi kufanyika shughuli nyingine yoyote katika uwanja wa kuchezea na eneo la uwanja wa ndani ya uzio wa ndani wa uwanja kama vile muziki, ujenzi na kuendeshwa kwa vyombo vya moto na visivyo vya moto"

"Hairuhusiwi kwa viongozi wa klabu, mashabiki na mtu yeyote asiyekuwa na kazi maalum kuhusiana na mchezo katika eneo la uwanja(pitch) kuwepo eneo la uwanjani ndani kuzunguka uwanja wa kuchezea(pitch)"

Kamati inatoa Onyo na angalizo kuwa kanuni hizo zisipozingatiwa uwanja huo utafungiwa mara moja

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’