Yanga iko Musoma tangu juzi ambapo jioni ya leo Jumapili itashuka katika uwanja wa Karume kuikabili Biashara United ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Huu ni mchezo muhimu kwa Yanga kuondoka na alama zote tatu ili kuendelea kujiweka vyema katika vita ya kuwania nafasi ya pili
Lakini pia, utakuwa sehemu ya maandalizi ya kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria kuelekea mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Jumapili ijayo
Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema wachezaji wake wanafahamu hautakuwa mchezo mwepesi hasa kutokana na mazingira ya uwanja wa Karume, hata hivyo watapambana kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu
Baada ya mchezo huo, Yanga itaelekea Kagera ambako inakabiliwa na mchezo mwingine mgumu dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Julai 09 katika uwanja wa Kaitaba