Kagera Sugar yaitega Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jul 2020
Kagera Sugar yaitega Yanga

Keshokutwa Jumatano, mabingwa wa kihistoria Tanzania Yanga watashuka kwenye uwanja wa Kaitaba kumenyana na Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Huu ni mchezo muhimu kwa Yanga kupata ushindi ili kuweka hai matumaini ya kumaliza ligi katika nafasi nzuri

Lakini pia ni mchezo ambao utachezwa siku chache kabla ya mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili ijayo

Ikumbukwe Yanga iliwaondoa Kagera Sugar katika mchezo wa robo fainali ambao ulipigwa uwanja wa Taifa wiki iliyopita, Yanga ikishinda mabao 2-1

Mchezo huo uligubikwa na matukio ya hapa na pale Kagera Sugar wakilalamika kuonewa na waamuzi

Hivyo Kagera Sugar watauchukulia mchezo wa keshokutwa kuwa wa kisasi hasa ikizingatiwa watakuwa wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani

Nyota wa Yanga watapaswa kuwa makini ili kuhakikisha hawapati majeraha katika mchezo huo ambao utakuwa na presha kubwa

Kocha Luc Eymael anaweza kulazimika kufanya mabadiliko ya kikosi chake ili kuhakikisha anawalinda nyota wake kuelekea mchezo dhidi ya Simba

Yanga wakiwa tayari wamempoteza Mapinduzi Balama, kuna hofu ya kumpoteza Haruna Niyonzima aliyepata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Biashara United jana

Majeruhi zaidi wanaweza kuiweka Yanga katika wakati mgumu zaidi kuelekea mchezo dhidi ya Simba

Yanga inahitaji kuifunga Simba ili kutinga fainali ya michuano ya kombe la FA kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
25m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’