Morrison awaambia Simba wajiandae 'kisaikolojia'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jul 2020
Morrison awaambia Simba wajiandae 'kisaikolojia'

Baada ya kuifungia timu yake bao pekee kwenye ushindi walioupata dhidi ya Kagera Sugar juzi, kiungo mwenye 'mbwembwe' wa klabu ya Yanga, Bernard Morrison amesema hizo ni salamu kwa wapinzani wao kwenye mchezo wa Jumapili wa hatua ya nusu fainali ya kombe la FA na kuwataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo

Yanga Jumapili itawakabili Simba kwenye hatua hiyo ya nusu fainali, mchezo unaosubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa timu hizo mbili.

Morrison, alisema kuwa goli alilolifunga linampa mzuka wa kufanya vizuri kwenye mchezo unaofuata na kuisaidia timu yake kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo ya FA.

Alisema mashabiki hawana haja ya kuwa na hofu na mchezo huo kwa kuwa yeye na wachezaji wenzake wanatambua umuhimu wa mchezo huo

"Lengo ni kufanya vyema na kuhakikisha tunacheza fainali ya FA, tunafahamu ndio tiketi yetu ya pekee kucheza mashindano ya kimataifa," alisema Morrison na kuongeza,

"Muda uliobakia naamini benchi la ufundi litaendelea kutuandaa na kutujenga kwa mchezo huo, tusubiri siku ifike," alisema.

Morrison ni kama ameamsha hisia za mashabiki wa Yanga kuelekea kwenye mchezo huo wa Jumapili kutokana na bao alilofunga dhidi ya Kagera.

Kabla ya mchezo huo kulikuwa na sintofahamu kwa mashabiki kujua mustakabali wa kiungo huyo kuelekea kwenye mchezo wao huo.

Ni wazi sasa uwepo wake kwenye mchezo huo utawapa shauku kubwa mashabiki wa Yanga kuelekea kwenye mchezo huo.

Mshindi wa mchezo huo atatinga hatua ya fainali na kuchuana na mshindi baina ya Sahare ya Tanga na Namungo ya Lindi watakaocheza nusu fainali nyingine.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’